TARIME: Kaka Amuua MDOMO wake wa Darasa la Kwanza Kisa Kupendwa na baba


Mniko Chacha (20) Mkazi wa Tarime, amemuua mdogo wake Hassan Chacha(7) mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Kitagutiti Kijiji cha Getenga Kata ya Mbogi Wilayani Tarime, kwa kumshambulia, kumning’iniza juu na kisha kumtupa chini

Chanzo cha kaka kufanya tukio hilo kimetajwa kuwa ni na mdogo wake kupendwa sana na baba yao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime /Rorya, Henny Mwaibambe amethibitisha tukio hilo ambapo amesema tukio hilo linasikitisha sana.

Alisema, kaka wa marehemu alimwambia marehemu kuwa kwanini wewe unapendwa sana, marehemu huyo ni mapacha Kurwa na Dotto, aliyefariki ni Dotto.

Mwaibambe amesema, ukiangalia umri wa mtoto huyo ni mdogo hivyo ni lazima apendwe tu na wazazi na kaka yao ni mtu mzima hakupaswa kufanya huo ukatili.

“Alimshambulia kwa kumning’iniza juu na kumtupa chini mara mbili akidai kwanini anapendelewa na baba yao kwa kuitwa mara kwa mara jikoni, marehemu alipata maumivu ambapo alikimbizwa katika kituo cha afya cha Dk. Steven na alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu,” ameongeza.

Aidha Kamanda Mwaibambe amesema kuwa mtuhumiwa alitoroka baada ya kutenda tukio hilo na juhudi za kumtafuta na kumkamata zinaendelea.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad