Timu ya Taifa Yaahidi Kwenda Kufanya Kweli Afcon

NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania anayekipiga KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta amesema kuwa wanatambua kazi kubwa waliyopewa na Taifa hivyo watakwenda Misri wakiwa na lengo moja kupata matokeo chanya kwenye michuano hiyo ya Afcon itakayofanyika kuanzaia 21Juni nchini Misri.

Akizungumza na Saleh Jembe, Samatta amesema kuwa muda wa miaka 39 iliyopita bila Taifa kuwa na mwakilishi ni lazima ilipwe hasa kwa timu kupata matokeo chanya ili kuwapa raha watanzania.

"Ninatambua kwamba watanzania wanapenda mpira ndio maana wanatupa sapoti, hivyo kazi yetu tuliyopewa tutaifanya kwa ukamilifu kwa kuwapa zawadi ya ushindi kwenye mechi zetu ambazo tutacheza kwenye michuano ya Afcon.

"Kila mchezaji anajua kazi yake hivyo kile ambacho tunakwenda kukifanya tunajua ni kwa ajili ya Taifa, tutapambana kwa kila namna kupeperusha Bendera ya Taifa kimataifa," amesema Samatta.

Stars ipo kundi C ikiwa na timu kama Kenya, Algeria na Senegal, mchezo wao wa kwanza ni dhidi ya Senegal inatarajiwa kuondoka leo kwenda Misri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad