TRA Yaanzisha Msako wa Kodi, Wasiotoa na Kudai Risiti Kupiga Faini

Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mkoa wa Kodi Kariakoo umetoa tangazo la kukamata mizigo au bidhaa ambazo hazitakuwa na risiti halali ambapo kwa wasiotoa risiti watatozwa faini ya Tsh. milioni 3 hadi milioni 4.5 na wale wasiodai risiti watatozwa faini ya Tsh. milioni 1.5 kwa kila kosa

Meneja wa Kodi Kariakoo Jijini Dar es salaam, Hashim Ngoda amesema kuwa TRA imeanza kuendesha msako katika maeneo yote kwa wale wasiotoa au kudai risiti wafanyapo manunuzi ya bidhaa mbalimbali

Katika hatua nyingine, aliwajulisha wamiliki wote wa majengo kuwa mwisho wa kulipa kodi ya majengo kwa mwaka 2018/19 ni Juni 30, mwaka huu

Utaratibu wa ulipaji wa kodi hizo kwa nyumba ya kawaida ni Tsh. 10,000, nyumba ya sakafu ya ghorofa katika majiji, miji na manispaa ni Tsh. 50,000 pamoja na ghorofa zima katika Halmashauri za Wilaya ni Tsh. 20,000 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad