Wanawake wawili wamesema wazi kuwa mwandishi wa E. Jean Carroll aliwatobolea siri baada ya Donald Trump kudaiwa kumbaka katika miaka ya 1990
Carol Martin na Lisa Birnbach wakati mwingine hawakubaliani juu ya ikiwa Bi Carroll angepaswa kuwaita polisi, imeeleza taarifa ya gazeti la New York Times.
Bi Carroll, mwenye umri wa miaka 75, ni mwanamke wa 16 kumshutumu Bwana Trump kwa tabia isiyofaa ya kingono.
Kansela wa Ujerumani atetemeka hadharani
Kansela wa Ujerumani atetemeka hadharani
Chifu Mkwawa: Shujaa aliyewatishia wakoloni Afrika mashariki
Bi Martin, ambaye alikuwa mtangazaji wa TV kati ya mwaka 1975-95,na Bi Birnbach, mwandishi , waliongea hadharani kwa mara ya kwanza kuhusu madai ya unyanyasaji wa kingono katika kipindi cha podcast cha gazeti la New York Times.
Bi Carroll, mwandishi wa ukurasa wa Elle, alisema kuwa katika kipindi hicho cha said in podcast alimuita Bi Birnbach mara moja baada ya madai ya kubakwa, akimwambia kuwa Bwana Trump alimlazimisha kufanya ngono.
Bi Birnbach alijibu kwa kusema kuwa alidhani kuwa ulikuwa ni ubakaji, akamtaka Bi Carroll awapigie simu polisi.
Trump matatani ukatili wa kijinsia
Trump amwomba radhi Jaji Kavanaugh
"Hebu twende polisi . Nitakupeleka polisi " Alisema Bi Birnbach , lakini akaongeza kuwa rafiki yake alikataa.
Bi Carroll alielezea kile kilichotokea baina yake na Trump kama "mapigano", si "uhalifu ".