''Tufanye Kama Rais Magufuli Anavyotuongoza''

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka waislamu kote nchini waendeleze utulivu, amani na uadilifu waliouonesha katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwani kwa kufanya hivyo, watasaidia kukuza umoja wa kitaifa, uchumi na kuboresha huduma za jamii.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Juni 5, 2019) kwenye Baraza la Eid El Fitri, lililofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Tanga Beach Resort jijini Tanga.“Nawashi sana kuyaenzi mema yote mliyoyafanya kipindi cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan’’.

"Rushwa ni dhambi kubwa na hukumu yake mbele ya Mwenyezi Mungu ni moto kwa sababu rushwa ni kipingamizi kikubwa cha maendeleo, hivyo tuungane pamoja kupinga rushwa ndani ya nchi yetu kama Rais Dkt. John Magufuli anavyotuongoza."

Amesema ni vema wakatambua kwamba uadilifu waliouonesha ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni silaha muhimu hususan katika kuimarisha maendeleo na kudumisha haki, umoja, usawa, upendo na utulivu.

Kadhalika, Waziri Mkuu amezipongeza taasisi za Kiislamu na imani nyingine ambazo zimejenga shule ili kuchangia maendeleo ya elimu kitaifa lakini amesisitiza kuwa bado kuna haja ya kuongeza shule nyingine na vyuo zaidi pamoja na kuziboresha zile zilizopo ili kusaidia jitihada za Serikali katika kuboresha huduma za jamii Nchini

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad