Ty Dolla Sign afutiwa mashtaka yake ya kukutwa na dawa za kulevya

Kwa mujibu wa mtandao wa The Blast umeripoti kuwa rapper Ty Dolla $ign amefutiwa mashtaka yote ya dawa za kulevya aliyowahi kufunguliwa mwaka 2018, hii ni baada ya kukamilisha darasa lake la mafunzo na elimu juu ya dawa za kulevya kama alivyokubaliana na Mahakama.

Inaelezwa kuwa baada ya Ty kuingia kwenye sakata hilo mwezi September 2018 na kukamatwa kwa makosa hayo ilibidi aingie kwenye makubaliano na waendesha mashtaka na kupanga kuwa endapo atafata masharti ya kukamilisha darasa hilo basi hana budi ya kufutiwa mashtaka yake yaliyokuwa yakimkabili.

Ty Dolla $ign alikamatwa September 2018 akiwa na wenzake sita katika mtaa wa Martin Luther King Jr. Dr Atlanta Marekani na kuelezwa kuwa Polisi walisikia harufu ya Marijuana pamoja na Cocaine Latina gari alilokuwa akiendesha Ty na ndipo hapo alipofunguliwa mashtaka hayo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad