Mpaka wa Tanzania unashikana na wa Congo, ambako virusi vya ugonjwa huo vimesababisha vifo vya takriban watu 1, 400.
Kauli hii inatolewa wakati Uganda imethibitisha kwamba kuna visa visaba vya watu wanaoshukiwa kuugua ugonjwa huo nchini.
Katika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter, Bi Mwalimu amesema Tanzania "imekuwa ikichukua hatua za utayari wa kukabiliana na ugonjwa huu"
Mpango huo utawasaidia maafisa kusambaza kwa haraka taarifa kuhusu iwapo kumegunduliwa visa vyovyote vya Ebola, waziri huyo ameeleza.
Nchini Uganda mtoto wa miaka mitano aliyepatikana na Ebola alifariki hapo jana , kikiwa ndicho kisa cha kwanza kuthibitishwa nchini humo.
mahujaji wa DRC wazuiwa kuingia Uganda kutokana na tisho la Ebola
Wizara ya afya nchini Kenya kwa upande wake imetoa taarifa ikisema imetoa tahadhari kwa maafisa wote wa afya na umma kushinikiza hatua za uangalizi.
Wizara hiyo imeeleza kwamba inaendelea kuufuatilia mlipuko huo wa muda mrefu katika jamhuri ya Kideokrasi ya Congo ulioanza mnamo Agosi mwaka jana, kwa lengo la kuimarisha utayari na muitikio wa wa Kenya katika kukabiliana na visa vya ugonjwa huo.