Ushauri Wangu Mdogo kwa MREMBO Wema Sepetu
0
June 27, 2019
Wema Mungu amekujalia sura ya kuvutia, wazazi waliokupatia mahitaji yako muhimu mpaka umefika hapo na pia umejaliwa Nyota ya kupendwa. Yachukulie haya kukujenga wewe.
Hapa duniani hakuna asiyefanya makosa, wengine tunalipia makosa yetu kwa gharama kubwa sana, cha muhimu ni kuakisi maisha yako na kuona ulikosea wapi.
Kuna watoto wasio na wazazi au walezi, Wema unaweza kulipa fadhila kwa Mungu kwa kukujalia wewe wazazi, unatafuta nyumba na kukusanya watoto ukawapa malezi mema, kuwapa matibabu na elimu. Hapa duniani utakumbukwa na ahera (kama ipo) utakuwa umejiwekea thawabu kubwa sana.
Wema umejaliwa nyota ya kupendwa. Miss Tanzania 2006 ni mtu ambae hachagui watu wa kujichanya nao. Mtoto wa balozi ungeweza kuwa na marafiki wa matawi tu, lakini Wema wewe ni wa kipekee, huchagui watu kwa hali zao. Wema ukifanya Fund Rising Dinner kwa kukusanya hela za kulelea watoto wa mitaani muitikio wake utakuwa mkubwa sana.
Wema wewe ni mtoto wa Kiislam, ni muda wa kumrudia Mungu, vaa kistara, haya mambo ya kuonyesha tatoo waachie wadogo zako. Tutafurahi tukisikia Wema amekwenda Mecca kuhiji na sasa amekuwa mtu wa swala tano au siku moja tusikie na yeye siku moja kateuliwa kuwa Kiongozi Kama Jokate
By Sky Eclat
Tags