Uturuki Yaunga Mkono RIPOTI ya Umoja wa Mataifa Mauaji ya Mwandishi wa HABARI wa Saudia
0
June 20, 2019
Wizara ya mambo ya nje ya Uturuki yaınga mkono ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya Jamal Khashoggi na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wahusika.
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu amesema kwamba wizara yake ina unga mkono ripoti ya Umoja wa Mataifa iliotolewa kuhusu mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi alieuawa katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul.
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki amesema kuwa ripoti hiyo iinaungwa mkono na Uturuki bila ya kipingamizi ili waliohusika na mauaji hayo wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.
Mevlüt Çavuşoğlu Jumatano ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuhusu ripoti iliotolewa na Agnes Callamard, ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya wanahabari Jamal Khashoggi.
Katika ujumbe wake huo, waziri wa mambo ya nje wa Uturuki amesema kuwa Uturuki inaunga bila kipingamizi ripoti hiyo ya UM.
Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa yenye kurasa 101 imeishutumu Saudia kuhusu na mauaji ya Jamal Khashoggi.
Ripoti hiyo imeendelea kufahamisha kuwa kuna ushahidi tosha kuwa mwanamfalme wa Saudia Mohammed Bin Salman na viongozi wengine wanatakiwa kuchunguzwa kuhusu mauaji hayo.
Tags