Waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang'i amewatimua nchini humo wafanyabiashara saba wa Kichina waliopatikana na hatia ya kufanya biashara zao kinyume cha sheria katika soko la maarufu kwa mitumba -Gikomba.
Hii ni baada ya Wakenya wanaouza bidhaa zao kwenye soko hilo lililopo jijini Nairobi kulalamikia ongezeko la Wafanyabiashara wa Kichina ambao walidai kuwa wanawaajiri wenzao na kuleta ushindani wa biashara.
Jumatano wiki hii Waziri wa mambo ya ndani alikuwa ameahidi kuwatimua wafanyabiashara wa kichina na wengine wa kigeni ambao watabainika kufanya biashara ndogo ndogo jijini Nairobi baada ya wakazi wa jiji hilo kulalamika kuwa Wachina wameleta ushindani mkubwa na wenyeji wanaofanya biashara katika masoko yanayouza nguo kuu kuu na bidhaa nyingine za bei za chini jijini humo ya Gikomba, Kamukunji na Nyamakima.
Waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang'i amewaonya wafanyabiashara wa kigeni wanaoendesha shughuli zao bila vibali kuwa hawana nafasi nchini Kenya
"Raia wa kigeni kandaa wanaoshukiwa kufanya biashara nchini Kenya walikamatwa wakati wakati wa msako wa uvamizi wa katika soko la Gikomba. Wachina saba walibainika kukiuka sheria za uhamiaji.Maafisa walibaini kuwa watatu kati yao hawakuw ana vibali vya kazi huku wengine wakifanya kazi na shughuli nyingine zinazowaingizia mapato kinyume na vibali walivyopewa walipoingia nchini ,"ilisema taarifa ya Wizara ya mambo ya ndani nchini kenya.
"kutokana na hayo, Waziri anayehusika na masuala ya uhamiaji ametia saini amri ya kuwarejesha makwao kulingana na sheria ."
Wachina wafukuzwa Kenya kwa kuuza bidhaa sokoni kinyume cha sheria
0
June 14, 2019
Tags