Wafanyabiashara wa Mifuko Mbadala Watakiwa Kutowakomoa Wananchi


Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mussa Sima amewataka wafanyabiashara wa mifuko mbadala kutotumia fursa hiyo kuwakandamiza wananchi kwa kuiuza kwa bei ya kubwa.

Sima ametoa kauli hiyo leo mjini Singida wakati aliposhiriki operesheni ya kukagua utekelezaji wa katazo la mifuko ya plastiki ambalo limenza Juni mosi mwaka huu.

Katika opresheni hiyo iliyoambatana na ugawaji wa mifuko mbadala iliyotolewa na Kanisa la Full Gospel kwa wananchi mjini hapo alisema ni busara kwa wafanyabiashara hao kuweka bei inayowawezesha wananchi kuweza kuinunua.

"Ndugu wafanyabiashara tusiwakomoe Watanzania wasije kuona sasa mifuko hii ni ghali na kuona ni bora turudi katika mifuko ya plastiki ambayo imepigwa marufuku," alisema.

Naibu Waziri Sima ambaye alikuwa mgeni rasmi katika operesheni hiyo akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi alisema wataalamu kutoka serikalini watatembelea viwandani kuona kama bei rafiki kwa mwananchi inatumika.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad