Wakazi Afichua Alivyosaidiwa Ingia Kwenye Hip Hop

MKALI wa michano Bongo, Wabiro Noel Wassira ‘Wakazi’ amefichua namna alivyoingia kwenye Muziki wa Hip Hop kwamba masomo ndiyo yalichangia.

Akizungumza na +255 Global Radio kupitia kipindi cha Bongo 255, leo Jumanne, Juni 4, Wakazi anayetikisa na vibao vingi kama vile Hapa Wakazi Tu na Kisimani alisema kuwa, kabla hajaingia kwenye muziki huo alipata nafasi ya kwenda kusoma Chicago nchini Marekani.

“Ujue wakati nimepata nafasi ya kwenda masomoni Marekani nilikuwa na ndoto za kufika mbali lakini pia nilitamani sana kuwa Mwanahip Hop. “Sasa nilipokuwa masomoni huko nikapata nafasi ya kuona hali halisi ya wasanii wakubwa hali iliyonisukuma kurudi Bongo na kufanya Hip Hop hadi leo hii,” alimaliza kusema Wakazi.

Wakazi pia aliongelea namna muziki wa Hip Hop ulivyo sasa tofauti na wazamani. “Sanaa au fasihi inajihusisha kutokana na nyakati uliopo. Zamani wasanii wote wakubwa walikuwa wanafanya Hip Hop lakini taratibu wanaoimba walikuwa wachache. Wakaanza kuchomoza hadi sasa wamekuwa wengi na wanaofanya Hip Hop kidogo.

“Hip Hop bado ina nguvu sema nyakati zinafanya isiwe maarufu. Watu wanasema muziki ni biashara kwa hiyo watu wa Hip Hop walikuwa wanazingatia biashara kama vile kuchezeka klabu, kuchanganya na kuimba na vinginevyo,” alimaliza kusema Wakazi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad