Wanafunzi Watakiwa Kuhakikisha Wanadahiliwa vyuo Vilivyosajiliwa


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William ole Nasha amewataka wanafunzi watakaoomba kujiunga na vyuo vya ufundi nchini kuhakikisha wanadahiliwa kwenye vyuo vilivyosajiliwa.

Nasha ametoa kauli hiyo,  wakati akifunga maonesho ya kwanza ya vyuo vya ufundi yalioandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE). Alisema tayari dirisha la udahili wa wanafunzi kwa kozi mbalimbali limeshafunguliwa na baraza hilo, hivyo ni vyema waombaji wakahakikisha wanaomba kwenye vyuo visivyosajiliwa na serikali.

"Elimu ya ufundi inahitajika kwenye soko la ajira kwa kuwa inaleta matokeo ya haraka, kwa muda mrefu watu wanafikiria elimu ni kuajiriwa badala ya kufikiria kuwa ni nyenzo tu ya kukuwezesha kujiajiri mwenyewe,"alisema.

Aidha, alituma fursa hiyo kuwaasa vijana wahitimu wa vyuo mbalimbali nchini kutumia elimu kama nyenzo ya kupambana na changamoto ikiwa ni pamoja na kujiajiri.

Alisema imefika wakati kwa vijana wa Kitanzania kuondokana na dhana ya kusubiri ajira mara wanapohitimu masomo yao, badala yake wafikirie katika kujiajiri mara baaada ya kuhitimu.

Pia alisema maonesho hayo yameamsha hali ya kushirikiana baina ya wadau na kubadili fikra kuwa wataalamu wa fani mbalimbali si lazima wawe wa kutoka nje ya nchi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad