Wanawake punguzeni midomo inawakimbiza wanaume kukaa nyumbani


Baadhi ya wanawake wamekuwa ni kero nyumbani na kusababisha wanaume kukimbia nyumba zao ama kwenda kushinda baa.

Hili sio jambo nzuri kabisa kama unajijua unatabia hizo naomba ujirekebishe maana italeta athari mbaya kwa baadaye.

Tujitahidi kuwa makini na midomo yetu wanaume wanapenda kubembelezwa kama watoto wadogo.

Jambo la msingi unalitakuwa kuzingatia ni kuutumia ulimi wako kuongea maneno mazuri sio kila wakati ni kuanzisha visa kila unapomuona maneno hayaishi.



Kuna baadhi ya wanaume utamsikia akisema mimi siendi nyumbani muda huu nitaenda kugombana na mke wangu.

Hii haiposawa tuwe makini kwani tunakimbiwa na wanaume nyumbani kwa sababu ya kuongea sana. Mimi napenda mume wangu arudi mapema nifurahi naye tuanze kuandaa mapema vyakula vyetu vya usiku huku akinipa raha.

Nakushauri napokuwa nyumbani jitahidi kumfanya mmeo mwenye furaha mpe raha zake atamani kubaki nyumbani hata akipigiwa simu na washikaji anajisikia uvivu kutoka.

Kitendo cha mumeo kukukimbia kukaa nyumbani na kwenda huko vijiweni ama katika baa ni kumuongezea mawazo na kutafuta mchepuko ili apate amani aliyokuwa anaikosa nyumbani.

Pia vitu vingine ambavyo wanaume hawapindi ni pale anaposhinda nyumbani matumizi ya fedha yanakuwa makubwa.



Wakina mama wengine sasa ni kero utakuta na yeye anafanya kazi na mwanaume ameacha hela ya chakula. Kisa unamuona kashinda nyumbani basi wewe ndio kila kitu unaagiza mtoto akafuate hela.

Umeona chumvi hakuna unamuita mtoto akadai hela mara sukari imesha mara kafuate hela ya mafuta. Hayo ni mambo ambayo wanaume wanakasirika.

Mwanaume mpaka anasema nikishinda nyumbani vitu vya jikoni vinaisha bora asiwe anashinda nyumbani.

Kama unajua vitu vyako vinakaribia kuisha mjulishe mwenzako mapema ili ajue jinsi ya kupanga bajeti zake za chakula.



Lakini jamani hata kama mwanaume ni jukumu lake la kuacha hela ya chakula hivi wewe mwanamke mwenzangu ambaye unafanya kazi unashindwa kweli kununua chumvi mpaka uanze kuagiza watoto wakadai hela kwa baba yao ya chumvi.

Hapana jamani tuache hizo tabia kununua kwa siku moja moja sio mbaya tunajishusha thamani kwa waume zetu na  kukutafsiri vibaya juu ya fedha zako.

Mambo hayo mawili wanaume wengi wamekuwa wakilalamika hivyo wanawake wenzangu tujirekebishe tunajitakia kupata michepuko kwa midomo yetu.

Ni vyema basi mwanamke akachunga kauli. Akawa si mtu wa kuchimbachimba vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Asiwe na kisirani. Kinywa chake kitawaliwe na maneno matamu, yatakayomtia moyo mpenzi wake, yatakayomfariji na yatakayomfanya apende kuzungumza naye.


Mara nyingi mwanaume akiona mke au mpenzi ni mtu wa kupenda chokochoko, mara nyingi humuepuka. Anajitahidi kadiri ya uwezo wake kukaa naye mbali. Ataona ni bora achelewe kurudi nyumbani akakutane na marafiki baa, wapige stori ili muda uende na akirudi nyumbani asiwe na muda wa kuzungumza na mwenzi wake, yeye ni kula na kulala.

Kama unaishi na mwanaume kazi yake ni kula na kulala hana mazungumzo na wewe jua anakuvutia kasi siku utakuacha mchana kweupe.

Wanaume wakichoka mauzi hawezi kuvumilia sio kama wanawake wanavumilia hawa husepa, hivyo jitahidi kuwa na kauli nzuri na mpenzi wako.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad