Wapenzi Wakutana Baada ya Kupotezana Tangu Vita ya Pili ya Dunia

Mwanajeshi mstaafu wa jeshi la Marekani KT Robbins, (97) ambaye alishiriki katika vita ya pili ya dunia amekutana na  mpenzi wake Jeannine Pierson,  92  mfaransa waliyepoteana kwa miaka (75), baada ya vita kuisha kukutana katika maadhimisho ya  D-Day.



Katika kiindi hicho cha vita Robbins akiwa kijana mwenye umri wa miaka 24 alikutana na Jeannine amabye umri wake ulikuwa ni miaka 18 katika mji wa  Briey uliopo kaskazini mashariki mwa nchi ya Ufaransa.



Baada ya Robinis kuondoka Ufaransa na kurudi Amerika, alikutana na mwanamke mwingine aliyeitwa Lilian na walioana na wakafanikiwa kuwa na familia yao hadi  mwaka 2015  Lilian aliofariki dunia akiwa na umri wa miaka 92.



Huku Ufaransa nako Jeannine pia aliata mwanaume mwingine ambaye alimuoa  na wakafnikiwa kuata watoto watoto watano.



Lakini katika kiindi hicho chote, Robbins anasema hajawahi kumsahau mpenzi wake Jeannine, na amezitunza picha zao ambazo walizipiga miongo kadhaa iliyopita, zenye rangi ya black and white.



Robbins aliamini kuwa Jeannine alishafariki na alipofika Ufaransa aliwaonesha waandishi wa habari Picha za Jeannine na kuwaomba akaombwa kwenda kuisabahi familia ya menzi wake huyo kwani hakutaraji kusikia kuwa  mwanamke huyo bado atakuwa anaishi.



Waaandishi wa habari walifanya upelelezi na kubaini kuwa Jeannine bado anaishi walimtafuta na wakakutana naye, wakamueleza kuhusu ombi la Robbins na mwanamke huyu aliwajibu kuwa yuu tayari kukutana nae na anamsubiri kwa shauku kubwa.


Cha ajabu na cha kufurahisha Robbins hakuamnini alipoambiwa Jeannine bado anaishi ndipo waandishi hao wakaanga tarehe na eneo la kuwakutanisha wakonghwe hawa hadi alipopelekwa na kukutanishwa naye uso kwa uso.

Walipokutana sasa, wakongwe hawa walikumbatiana na kubusiana kwa furaha huku Robbins akimuonesha  Jeannine picha walizoiga enzi za ujana wao.

Baada ya masaa kadhaa kupita Robbins alilazimika kuondoka kwa ajili ya kwenda kuhudhulia  katika sherehe za maadhimisho ya kumbukizi ya D-Day huko Normandy


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad