Wachunguzi wa kimataifa leo wamewafungulia watu wanne mashitaka ya kuua kuhusiana na kudunguliwa ndege ya abiria ya Malaysia MH17 mwaka wa 2014 katika anga ya eneo linalodhibitiwa na waasi la mashariki mwa Ukraine ambapo watu 298 waliuawa.
Timu hiyo ya Uholanzi imesema itawashitaki raia wa Urusi Igor Girkin, Sergey Dubinskiy na Oleg Pulatov, na Leonid Karchenko raia wa Ukraine kuhusiana na kuangushwa ndege hiyo ya Malaysia.
FRED WESTERBEKE, ni mwendesha mkuu wa mashitaka wa Uholanzi. Jamaa za wahanga wamesema kuwa wameambiwa kesi za watuhumiwa hao zitaanza Machi 2020, ijapokuwa kuna uwezakano watashitakiwa bila wao kufika mahakamani kwa sababu Urusi haina utaratibu wa kuwahamisha raia wake kwa ajili ya kushitakiwa katika nchi za kigeni.
Urusi inakanusha vikali kuhusika kabisa na tukio la kuangushwa ndege hiyo.