Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amesema Serikali imeshawasiliana na Ubalozi wa Marekani nchini kuhusiana na taarifa ya tishio la kushambuliwa katika baadhi ya maeneo jijini Dar es salaam.
Waziri Lugola ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuhusiana na tahadhari hiyo iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani na kupelekea kuzua hali ya taharuki jana hasa kupitia mitandao ya kijamii.
Waziri Lugola amesema kuwa "hii tahadhari iliyotolewa na wenzetu Marekani ni taarifa ya kawaida, kama wenzetu wamezipata na tumewailiana nao kupitia polisi, niwahakikishie watanzania wasiwe na hofu au wasiwasi, vyombo vyetu vinafanya kazi yake, hii ni tahadhari za kawaida kama ilivyo tahadhari za Tsunami, Mvua nyingi. n.k"
Jana akizungumza na www.eatv.tv Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, (ACP) Mussa Taibu ambaye aliweka wazi kuwa wamejipanga na kuimarisha usalama.
'Tumejipanga na vikosi vyetu kama kawaida kuhakikisha tunaimarisha usalama wetu na tunahakikisha maeneo yote yana usalama wa kutosha na sio wka hili tu, muda wote vikosi vyetu vipo tayari'', amesema Kamanda Taibu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ubalozi wa Marekani, maeneo yanayohofiwa huenda shambulio likafanyika ni Masaki katika hoteli na migahawa.