Waziri Mkuu wa Ethiopia Abey Ahmed Aingilia kati Mgogoro wa Sudan

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amewasili mjin Khartoum leo kujaribu kuupatanisha watawala wa kijeshi na makundi ya upinzani.

Viongozi wa makundi yanayopigania uhuru na mabadiliko -nayayotaka demokrasia nchini humo yamekataa mazungumzo zaidi na yametoa wito wa kuvunjwa kwa kikosi cha uingiliaji kati cha wanamgambo- Rapid Support Forces ambacho wanakishuhtumu kuwauwa mamia ya watu.

Wanasema kuwa jeshi lazima likabidhi mamlaka mara moja kwa kwa mamlaka ya kiraia ya mpito.

Kwa miezi kadhaa sasa, baraza la utawala wa mpito la kijeshi nchini Sudan limekuwa na utashi mzuri wa kuwa na ushirikiana na mataifa.

Lakini kutokana na taarifa za mauaji ya waandamaji Jumatatu na kuendelea kwa mateso na vitisho dhidi ya raia kumekuwa na laana dhidi ya utawala wa mpito wa kijeshi.

Muungano wa Afrika tayari umekwitoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi juu ya mauji ya hivi karibuni na imetishia kuwawekea vitisho maafisa binafsi wanaokwamisha mchakato wa kipindi cha mpito kuelekea demokrasia.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anaangaliwa kama mwana mageuzi na alikwishakutana na baraza la jeshi awali.

Hata hivyo utatakiwa kuwepo ushawishi mkubwa katika makubalino na Majenerali ili kuweza kuanzishwa kwa mazungumzo mapya ya uundwaji wa serikali.

Muungano huo wa Afrika umetaka uchunguzi kufanywa kuhusu mauaji hayo ambayo yanadaiwa kutekelezwa na vikosi vya usalama.

Tume hiyo inasema kuwa marufuku hiyo ilikubaliwa na wanachama na itaanza kutekelezwa mara moja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad