NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Damas Ndumbaro amesema kuwa ugomvi kati ya Marekani na China ni wa kibiashara hivyo Tanzania haiwezi kuingilia na kwamba itaendelea kufanya kazi/biashara na nchi zote hizo mbili bila matatizo.
Dkt. Ndumbaro ambaye ni mbunge wa Songea Mjini (CCM) amesema hayo leo Ijumaa, Juni 8, 2019 wakati akifanya mazungumzo maalum na kituo cha +255 Global Radio alipotembelea ofisi za Global Group, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.
“Ugomvi wa Marekani na China ni wa kibiashara, China anauza Marekani Dola milioni 400, Marekani anauza China bilioni 100, hii inatengeneza deficit au trade imbalance ya dola milioni 300, kwa hiyo China anauza zaidi na uchumi wake unakua kwa kasi, ukiona hivyo maana yake uchumi wako hauwezi kuwa mkubwa miaka kadhaa ijayo.
Shigongo (kushoto) akiongozana na Ndumbaro (katikati), Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (nyuma yao katikati), Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally (wa pili kushoto) na Kiongozi wa Global TV Online, Abdallah Ganzi (kulia).
“Kutokana na hilo, tangu enzi za Mwalimu Nyrere kuna misingi ambayo taifa letu limejengwa, kwanza sisi hatuchaguliwi rafiki na hatuwezi kuingilia ugombvi wao, tunafanya biashara na hao wote kwa kufuata taratibu na sheria zilizopo.
…Dkt Ndumbaro akisalimiana na wafanyakazi wa Global Group.
“Niwasihi Watanzania tuchukue vita hii ya kibiashara kama somo, tunaona fahari kutumia bidhaa kutoka nje, ili tupunguze hiyo naksi ya kibiashara tunatakiwa kupenda vya kwetu zaidi. Mzani wa biashara kati yetu na Kenya umekua. Tumepunguza naksi hiyo ya biashara na jana Rais Dkt. John Magufuli alitoa takwimu, tuachane na kuagiza vitu ambavyo hata kwetu vinapatikana,” amesema Ndumbaro.
…Akisani kitabu cha wageni.
Akifafanua zaidi alisema, kampuni ya Google ya Marekani imeshapiga marufuku Kampuni ya teknolojia ya China, Huawei, kutumia mfumo wa Android kwenye simu zake, jambo ambalo limefanya na wao kuanza kutengeneza mfumo wao huku Wachina wakipasua baadhi ya vifaa vinavyozalishwa na kampuni ya Apple.
Akizngumzia kwa mapana wigo wa biashara duniani, alisema Urusi imesaini mkataba na Kampuni ya Huawei ya China kwa ajili ya kujenga miundombinu ya intaneti ya 5G nchini humo. Hatua hiyo inakuja wakati Marekani ikizuia taasisi zake kufanya kazi na Huawei, kwa madai ya kuhatarisha usalama wa taifa kwa kutumia teknolojia yake ya 5G.
…Mhariri wa Championi Jumatatu, Ezekiel Kitula (kushoto) akiongea jambo wakati wa kumtembeza waziri huyo sehemu mbalimbali ofisini.
Rais Xi Jinping wa China ameshatangaza habari ya kutiwa saini mapatano ya kufutwa kwa matumizi ya sarafu ya Marekani katika miamala ya kibiashara ya nchi yake na Urusi huku Wizara ya Elimu nchini China ikitoa onyo kwa wanafunzi wenye uraia wa China wanaopanga kujifunza nchini Marekani kujitayarisha kukabiliana na sheria kali za kupata Visa.
Katika kujihami, alisema China imetangaza kuongeza ushuru wa bidhaa za mabilioni ya dola kutoka Marekani wakati ikijitayarisha kuchapisha orodha mbaya ya kampuni za kigeni, hatua ambayo wachambuzi wanasema inalenga kuiadhibu Marekani na kampuni za kigeni.
Amefafanua kwaba Marekani na China zimekuwa katika mvutano kuhusu uvumbuzi wa 5G ambapo Marekani inafanya kila liwezekanalo iwe ya kwanza kutumia ‘network’ hiyo kwani itatengeneza ajira milioni tatu, itaongeza TZS quadrilioni 1.148 katika GDP na kuipa uwezo wa kutawala mambo yote yanayofanyika mitandaoni.
“China imesema itaongeza ushuru kwa bidhaa za thamani ya dola bilioni 60 kuanzia Juni 1 kwa 5% hadi 25%, ni baada ya Marekani kuongeza ushuru kwa bidhaa za China za thamani ya dola bil. 200,” alisema.
Picha na Amos Nyanduku | + 255 Global Radio