Wizara ya Elimu Yampa Agizo Hili Mkurugenzi Mkuu wa Veta

Serikali kupitia Wizara ya Elimu imemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa chuo cha VETA kuongeza kasi ya kukitangaza chuo hicho.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Ole Nasha pamoja na hayo amesema kuwa VETA nchi nzima kunakuwa na utaratibu wa kutangaza nafasi za masomo katika vyuo hivyo.

Mbunge Mariam Kishangi ameuliza kuwa , Kipawa kuna chuo kikubwa cha Veta, hatujawahi kuona matangazo ya elimu inayotolewa, Je Serikali ina mpango gani wa kukitangaza chuo?

"Chuo cha VETA Kipawa naomba nimuhakikishie Mbunge nchi nzima kunakuwa na utaratibu wa kutangaza nafasi za masomo katika vyuo vyake vyote kama Mh. Mbunge anaona haitoshi kutangaza .Namuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Veta aongeze kasi na wigo ya utangazaji na wa nafasi mbalimbali za masomo ya Veta," amesema Nasha leo Bungeni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad