Zitto Afunguka Kuhusu Taarifa Zinazotumwa Kwenye Ukurasa wake Adai Msaidizi wake Ametekwa Ataka Wamuachie Wamteke Yeye

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe akizungumza bungeni hii leo ameeleza kuwa taarifa zinazowekwa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii sio za kwake.

Zitto ameeleza kuwa msaidizi wake Raphael Ongangi ametekwa na watu wasiojulikana kwa siku kadhaa sasa na amekwishatoa taarifa. Amesisitiza kuwa watekaji wamuachie Raphael na wamteke yeye ili wamalizane vizuri.

“Nimekwishatoa taarifa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola kwamba juzi msaidizi wangu alitekwa na Watu wasiojulikana, najua lengo sio yeye na sasa mitandao yangu ya kijamii kuna jumbe zinatolewa ambazo sio zangu, niwaombe waliomteka wamuachie waje waniteke mimi” amesema Zitto.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad