Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo/Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kazi ya kuuza sio kazi ya Wizara ya Biashara ila kazi yake ni kuwezesha ila sekta binafsi ndio yenye mamlaka ya kuweza kuhakikisha kwamba bidhaa zinauzwa au laa.
Zitto katika Mkutano wake na Waandishi wa Habari alisema kuwa "Rais alieleza sababu za kumuondoa Waziri wa Viwanda na Biashara ni kwasababu hajauza Korosho, alisema hakuna sababu ya kuwa na Wizara kama Korosho haziuzwi kwanza tunataka kuweka wazi tatizo la Korosho hili tatizo lilityengeneza na mtu mmoja anaitwa John Pombe Magufuli asitafute watu wa kuwapa lawama maamuzi ya hovyo kuhusu Korosho yalipaswa kubebwa na Mkuu wa nchi mwenyewe ."
"Maamuzi aliyoyaelekeza hakuna Waziri ambaye angeenda kinyume na maelekezo yake lakini pili kazi ya Wizara ya Viwanda na Biashara sio kufanya biashara ya kuuza, kazi ya viwanda na biashara ni kufanya facilitation (kuwezesha) sekta binafsi ndio yenye mamlaka ya kuweza kuhakikisha kwamba bidhaa zinauzwa au laa."