Zitto Kabwe Asifu Msimamo wa Serikali

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesifu msimamo wa Serikali ya Awamu ya Tano kwa miaka mitatu mfululizo kuhusu miradi yake mitatu mikubwa iliyoianzisha.


Zitto ambaye pia ni Kiongozi wa Chama Cha ACT-Wazalendo, ametaja miradi ambayo Serikali imeonesha kuwa na msimamo mkali kuwa ni pamoja na ununuzi wa ndege za Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), mradi wa umeme wa Mto Rufiji (Stiegler’s Gorge) na Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR).


“Kuna jambo tuliweke wazi, Serikali imekuwa na msimamo mkali kwenye miradi yake. Tangu bajeti ya kwanza ya mwaka 2016 kuna ununuzi wa ndege na ujenzi wa reli. Bajeti ya mwaka 2017, fedha za reli ziliongezeka na tukaanza kutenga fedha kwa ajili ya mradi wa umeme,” Zitto anakaririwa na Mwananchi.


Hata hivyo, mwanasiasa huyo ameeleza kuwa kuna changamoto ya miradi hiyo kutoingiza fedha kwenye mzunguko wa uchumi.


Mjadala mkubwa hivi sasa ni mradi wa Stiegler’s Gorge ambao umezua gumzo hasa baada ya mataifa ya Magharibi kueleza kuwa unaharibu mazingira kwa kukata miti milioni mbili.

Msimamo wa Serikali ni kuhakikisha mradi huo unakamilika kwani utakuwa suluhisho la tatizo la umeme nchini na kama alivyosema Askofu wa Ufufuo na Uzima, Dkt. Josephat Gwajima ‘ili ule chips mayai ni lazima uvunje baadhi ya mayai uliyonayo’.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad