12 washikiliwa kwa kununua Madini ya dhahabu nje ya soko wilayani Kahama .....Wazari Bitteko atoa maagizo mazito


Waziri wa Madini Dotto Biteko ,amegiza kukamatwa   kwa wanunuzi wa madini 12  (Brokers) kutoka katika kata ya Kakola, Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga waliotajwa kuwa vinara wa  ununuzi  wa madini aina ya dhahabu na kuikosesha serikali mapato.

Uamuzi huo ameutoa jana baada ya kufanya ziara ya kushitukiza kwa baadhi ya ofisi za wanunuzi hao katika kijiji hicho na kubaini baadhi yao wakiendelea kununua dhahabu kwa wachimbaji wadogo bila nje ya soko ambalo kwa wilaya ya kahama soko hilo lipo katika ofisi ya madini.

Katika ziara hiyo  Bitteko ameagiza kukamatawa na kuhojiwa kwa mnunuzi wa dhahabu Sitta Kashepa baada ya kunununua dhahabu kilo 3  yenye thamani ya shilingi milioni 300  huku mwingine akinunua kilo 2.64 na kuuza kiasi cha shilingi Milioni 241 na wote wakiwa hawajalipa kodo ya serikali

Amesema katika ziara hiyo wamebaini kiwanda kimoja cha uchenjuaji wa madini ambacho kilikuwa kimefungwa na serikali kikiendelea kufanya kazi huku viongozi wa ofisi ya madini wakiwa hawana taarifa na wahusika wakiwa wamekata utepe maalumu uliowekwa na maafisa madini(seal).

“Haiwezekani maafisa wetu kutokuwa na taarifa hizi ambazo zinaonesha kuwepo kwa vitendo vya uhujumu uchumi unaofanyawa na wanunuzi hawa mpaka wizara itume tume maalumu kuja kubaini madudu haya”alisema Bitteko

Katika hatua nyingine  Waziri Biteko ametoa zawadi ya Shilingi milioni mbili kwa mtoa taarifa zilizofanikisha wanunuzi hao kubaini ambao wengi wao wamefahamika kuyauuza madini hayo katika nchi za Kenya na uganda na kuiagiza kamati ya ulinzi na uasalam ya wilaya kumtambu na kumthamini.

Amesema serikali haitasita kuchukua hatua kali kwa maafisa madini katika ofisi ya wilaya ya kahama baada ya kutotimiza majukumu yao baaada ya ofisi yake kubaini baadhi yao kuhusika katika uhujumu wa mapato kwa kushirikiana na wanunuzi hao kwani wamebaini uwepo wa majiko mbalimbali katika eneo hilo kuwepo katika makazi yawatu huku mengine yakiwa hayana usajili na yakiendelea na uchomaji wa dhahabu.

Amefafanua serikali ya awamu ya tano chini Rais Magufuli imepunguza kodi za madini kutoka asilimia 17 hadi 7 lakini baadhi ya wanunuzi wa madini bado hawataki kutii agizo hilo na kuendelea na utoroshaji ambao usipothibitiwa utaendelea kuikosha serikali mapato yatokanayo na mirahaba na kodi ya ushuru wa huduma(service leavy).


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad