ACT Wazalendo wasusia uchaguzi wa jimbo la Lissu


Chama cha ACT Wazalendo kimesema hakitashiriki uchaguzi mdogo uliotangazwa katika jimbo la Singida Mashariki Julai 31 Mwaka huu kwa madai ni haramu.

Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, amesema hayo leo kuwa msimamo wao wa chama chake wamefadhaishwa na hatua za Spika Job Ndugai kumfuta ubunge Tundu Lissu.

“Sisi hatutaweza kushiriki uchaguzi huo haramu msimamo wetu ndio huo tukishiriki maana yake ni kubariki haramu hatupo tayari katika hilo,” amesema.

Juni 28 mwaka huu Spika Ndugai alitangaza kumvua ubunge Lissu wakati akiahirisha bunge la bajeti.

Ndugai alitangaza uamuzi huo wa kumvua ubunge Lissu kwa ku​muandikia barua mwenyekiti wa NEC kumtaarifu kuwa kiti cha ubunge jimbo la Singida Mashariki kipo wazi akisema Lissu amepoteza sifa za kuwa mbunge kutokana na sababu mbili ambazo ni kutokuwepo bungeni bila taarifa na kutokujaza fomu ya tamko ya mali na madeni.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad