Agrey Moris Nje ya Uwanja Wiki Nane

Agrey Moris Nje ya Uwanja Wiki Nane
Nahodha wa Azam FC, Agrey Moris, anatarajia kuwa nje dimba kwa muda wa miezi miwili ijayo baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti nchini Misri.

Moris aliumia kwenye mchezo wa kirafiki wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' dhidi ya Misri wakati ikijiandaa na michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) inayoendelea kutimua vumbi nchini humo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Daktari wa Azam FC, Mwanandi Mwankemwa aliyekwenda nchini humo kushugulikia matibabu yake, beki huyo kisiki alikuwa na uvimbe kwenye kisahani kidogo juu ya goti (patella) na kuchanika kidogo kwa mtulinga wa pembeni wa goti lake.
.
.
"Agrey amefanyiwa operesheni kuondoa uvimbe huo na kufanyiwa 'repair' kwa mtulinga wa pembeni wa goti lake na ameelekezwa mazoezi ya kufanya kwa wiki mbili, baada ya siku 14 kutoka alipofanyiwa upasuaji atatolewa nyuzi na ataanza mazoezi ya gym moja kwa moja," imeeleza taarifa hiyo.

Mwankemwa amesema kuwa baada ya siku 21 (wiki tatu) tokea afanyiwe upasuaji, mchezaji huyo mwandamizi wa Azam FC ataanza mazoezi ya kukimbia kidogo kidogo huku akitarajia kurejea dimbani kwa ajili ya ushindani baada ya siku 60 kupita.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad