Algeria Yawa Bingwa Yailaza Senegal Kombe la Mataifa ya Afrika Afcon 2019
0
July 20, 2019
Algeria imeshinda kombe la mataifa ya Africa kwa mara ya pili baada ya kujipatia goli la mapema dhidi ya Senegal katika fainali iliochezwa mjini cairo.
Shambulio la Baghdad Bounedjah lilimgonga mchezaji wa Senegal Salif Sane na kupita juu ya mlinda langgo Alfred Gomis
Senegal, ambao hajawahi kushinda michuano hiyo , walipewa penalti baada ya mchezaji wa Algeria kuunawa mpira katika kipindi cha pili lakini refa wa video VAR alibadilisha uamuzi huo na kusema penalti haikufaa kutolewa.
De Ligt safarini kukamilisha usajili na Juventus
Algeria ilitumia kila mbinu kuwazuia wachezaji wa Senegal waliofanya mashambulizi ya kila aina ili kushinda kombe hilo tangu 1990.
Senegal ambao walikuwa wakishiriki kwa mara ya pili katika fainali tangu 2002 , walitawala kipindi kikubwa cha mechi lakini wakashindwa kuzalisha matunda.
Wachezaji wa Senegal walimwaga machozi baada ya kipyenga cha mwisho.
Mshambuliaji Sadio Mane alionekana kuwa na huzuni wakati wachezaji wa Algeria walipokuwa wakishangilia karibu yake.
''Bila wachezaji mimi si kitu,'' alisema Kocha wa Algeria Djamel Belmadi. ''Wao ni muhimu. Ninafikiri walicheza vizuri kwa nafasi yao na walipokea maelekezo vizuri sana.''
Tags