Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewasili nchini na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, wilayani Chato.
Uhuru Kenyatta anakuwa Rais wa kwanza wa kutoka nje ya nchi kukanyaga Chato ambapo ameeleza furaha yake kufika hapo huku akisisitiza ushirikiano wa nchi hizo mbili.
"Sisi kama watoto wa EAC lazima tufanye yote tunayoweza, ili kuondoa vikwazo vyote vinazuia watu wetu kutembeleana, kufanya biashara, kuoana, na njia nzuri ya kumaliza ukabila ni kuruhusu watu kuoana, ili mtoto akizaliwa usijue kwao ni wapi," amesema.
Ameendelea kwa kusema, "Kitu nachopenda kama Rais wa Kenya ni kuona Wanaafrika Mashariki tuko pamoja, unasikia wengine wanaropoka mambo mengi ambayo hayapo, unawezaje kumwambia Mtanzania huwezitembea Kenya, au kumzuia Mkenya kuja Tanzania kufanya biashara"..
Facebook Twitter Google+ Pinterest