Amber Lulu Aeleza Ujio wa Mtoto..Amkejeli Mpenzi Wake wa Zamani Young Dee


Msanii wa Bongo Fleva, Amber Lulu amedai kuwa kwa sasa 'level' zake sio sawa na wapenzi wake wa zamani Young Dee na Prezzo, na ametuhabarisha kwasasa yeye ni mjamzito.

Amber Lulu amefunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, kupitia kipindi cha "FNL" baada ya kuulizwa kuhusu rapa Young Dee ambaye yupo nchini Marekani kwa sasa.

''Mimi sio mtu wa kumuongelea Young Dee, sasa hivi mimi ni mtu wa kumuongelea Jay Z, Omarion, Chris Brown na Wiz Khalifa, sina muda wa kumuongelea mtu ambaye nishamkanyaga, hata hapa siwezi kumuongelea Prezzo ni babu kashazeeka sio 'level' zangu."

Amber Lulu pia ameweka wazi ujio wa mtoto mpya baada ya kuonekana tumbo lake kuwa kubwa ambapo alisema, ''mimi ni mzuri, ukiniangalia juu mpaka chini, achana na kitambi huyu ni mtoto wenu mpya anakuja''.

Pia Amber Lulu amesema yeye ndio msanii wa kwanza wa kike kutoa milioni kumi kwenye video, hana shida na gari pesa hizo angekuwa msanii mwingine angenunua hata gari, bado anatembea kwa miguu na bajaji.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad