Askari nane wa jeshi la polisi ambao walishtakiwa kwa kosa la kusindikiza shehena ya dhahabu imefutwa na taratibu za kuwarejesha kazini tayari zimeanza.
Kadhalika, zimefutwa kesi 70 zilizokuwa kwenye gereza kuu la Butimba baada ya Rais John Magufuli kutembelea gereza hilo mkoani huko.
Askari hao walifunguliwa kesi namba moja ya uhujumu uchumi ya mwaka 2019 katika Mahakama ya Mwanza.
Waliofutiwa kesi hiyo ni Mkuu wa Oparesheni mkoa wa Mwanza, Morice Okinda, E 6948 D/CPL Kasala, F 133 PL Matete, G 6885D/C Alex, G 5080 D/C Maingu, G 7244D/C Timothy, G 1876 D/C Japhet na H 4060 DC David Kadama.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), Biswalo Mganga, akati akizungumza na waandishi wa habari kuwa ameifuta kesi hiyo kutokana na maslahi ya Taifa.
“Nieifuata kesi hiyo kutokana na kwamba ina mambo mengi yanayohusu maslahi ya taifa ila kuna kesi nyingine inayohusu dhahabu na watuhumiwa wawili watafutiwa kesi hiyo na wengine wataendelea,” alisema.
Awali askari hao walifikishwa katika Mahakama ya Mwanza Januari 11 mwaka 2019 pamoja na wafanyabiashara wane wakikabiliwa na makosa matano ya kutakatisha fedha, uhujumu uchumi na kula njama ya kupanga uhalifu.
Makosa hayo wanadaiwa kuyatenda kati ya Januari 4 na 5 mwaka huu.