Askari Nane Waliodaiwa Kusafirisha Shehena ya Dhahabu Wafutiwa Mashtaka
0
July 18, 2019
Kesi ya uhujumu uchumi namba moja ya mwaka 2019 inayowakabili askari nane walioshtakiwa kwa kosa la kusindikiza shehena ya dhahabu imefutwa na taratibu za kuwarejesha kazini kuanza.
Mkurugenzi wa mashtaka nchini Tanzania (DPP), Biswalo Mganga akizungumza na waandishi wa habari amesema kesi hiyo imefutwa kwa sababu ya maslahi ya Taifa.
"Nimeifuta kesi hiyo kwa sababu ya maslahi ya Taifa kwani kuna mambo mengi yanayohusiana na Taifa, lakini ipo kesi nyingine inayohusiana na dhahabu na watu wawili watafutiwa kesi hiyo na wengine wataendelea," amesema Mganga.
Askari hao ni Mkuu wa Operesheni mkoa wa Mwanza, Morice Okinda, E 6948 D/CPL Kasala, F 1331 PL Matete, G 6885 D/C Alex na G 5080 D/C Maingu.
Wengine ni G 7244 D/C Timothy, G 1876 D/C Japhet, H 4060 D/C David Kadama ambao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Januari 11, 2019.
Askari hao pamoja na wafanyabiashara wanne walikuwa wakikabiliwa na makosa matano ya kutakatisha fedha, uhujumu uchumi na kula njama za kupanga uhalifu, makosa waliyodaiwa kuyatenda kati ya Januari 4 na 5, 2019.
Tags