Baada ya Uhuru Kenyatta Naye Museveni Kutua Chato Leo

Rais wa Uganda Yoweri Museveni anatarajiwa kuzuru nchini tanzania leo Jumamosi kwa ziara ya siku moja ya kibinafsi ambapo atakutana na rais wa tanzania John Pombe Magufuli nyumbani kwake huko Chato.

Kulingana na taarifa iliotolewa na ikulu na kutiwa saini na mkurugenzi wa mawasiliano Gerson Msigwa viongozi hao wawili watafanya mkutano a faragha.

Ijapokuwa kuwa ni mkutano wa kuongeza udugu miongoni mwa viongozi hao ajenda ya mkutano huo unatarajiwa kuangazia maswala ya kibishara husuasana katika jamii ya Afrika mashariki.

Watu kadhaa wauawa baada ya al-Shabab kuvamia hoteli
Uturuki yaikaidi Marekani kwa kujihami na makombora ya Urusi
Familia za waliofariki ajali ya Boeing zadanganywa kuhusu fidia
Rais Museveni ni kiongozi wa pili kutoka kwa jamii ya Afrika mashariki kumtembelea rais Magufuli huko Chato wiki moja tu baada ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kuwasili nchini humo ili kumtembelea.

Vikwazo vya kibiashara
Katika mapokezi yake, Rais Uhuru Kenyatta alieleza furaha yake kujumuika na Watanzania na kumshukuru rais Magufuli kwa mualiko wake.

Alisema dhamira ya ziara hiyo ilikuwa kuimarisha uhusiano wa kijirani baina ya Kenya na Tanzania.

Haki miliki ya pichaIKULU
Alielezea umuhimu wa viongozi kuwajibika ili kuondosha vikwazo vinavyozuia biashara, kuruhusu mzunguko huru wa watu na kuzidi kuimarisha uhusiano na kusisitiza umuhimu wa mataifa ya Afrika mashariki kushikana kama kitu kimoja.

Kwa upande wake, mwenyeji rais John Magufuli alisisistiza lengo la taifa lake kuendelea kutunza uhusiano wa kieneo.

Rais Magufuli kwa sasa yuko katika likizo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad