Baada ya Ukimya Mrefu Wema Arudi na Wema Empire

BAADA ya kuwa kimya kwa kipindi, muigizaji ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu amefika katika Viunga vya Global Group, Sinza Mori jijini Dar na kuanika sababu za ukimya wake huku akitambulisha kampuni yake mpya ya Wema Sepetu Empire.



Akizungumza mapema leo ndani ya +255 Global Radio, Wema aliyekuwa ameongozana na dairekta wake, Neema Ndepanya alisema kuwa ukimya wake ulikuwa ni sababu ya kujipanga kuja na tamthiliya kubwa ambayo itakuwa chini ya Wema Sepetu Empire.


Wakiendelea na mahojiano.

“Wema Sepetu Empire ni kampuni ambayo ipo chini ya Endless Fame inayosimamia filamu zangu kwa muda mrefu. Siku zote naamini katika kula na wenzangu mimi siyo mchoyo hata marehemu Kanumba (Steven) aliniona na kunipa hii nafasi kwa nini nisimpe mtu mwingine hii nafasi, mimi ni mwanadamu halafu ni mwanadamu mzuri, tatizo watu tu!


“Mtaani kuna wasanii wachanga wengi hawajui wanaanzia wapi wanaenda wapi? Nilikuwa napokea simu hata 200 hadi 300 kwa siku moja kutoka kwa hawa wasanii wachanga wakiniomba niwasaidie.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad