Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amekumbusha juu ya wakimbizi waliokufa wakati wakiwa njiani kuelekea barani Ulaya.
Papa Francis amesema wale wenye dhiki wanastahili kusaidiwa. Ameeleza kuwa wahamiaji ni ishara ya watu wanaozingatiwa kama mabaki ya mwisho katika dunia ya sera ya utandawazi.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki alitoa nasaha hizo alipoongoza misa kwenye Kanisa la Mtakatifu Petro katika mwaka wa 16 tangu pale papa alipotembelea kambi ya wakimbizi katika kisiwa cha Lampedusa.
Kisiwa hicho ndicho mara kwa mara kinakuwa kituo cha meli zinazowasifirisha wakimbizi. Hata hivyo Waziri wa Mambo ya ndani wa Italia Matteo Salvini anazipiga marufuku meli hizo kutia nanga kwenye fukwe za kisiwa hicho.