Balozi wa Uingereza nchini Marekani ajiuzulu

Balozi Kim Darroch anayewakilisha Uingereza nchini Marekani, amejiuzulu yakiwa ni matokeo ya kuvuja kwa barua pepe zinazoukosoa utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump.

Balozi huyo, aliitwa ''mtu mpumbavu'' na Rais Trump, baada ya barua pepe hizo kusema utawala wa Trump si stadi''.

Ofisi ya mambo ya nje imesifu hatua ya Balozi Kim ''kwa weledi wake''

Balozi huyo amesema anataka kumaliza mzozo uliokuwepo na kuongeza kuwa kuvuja kwa barua pepe kumefanya utenda kazi wake kuwa ''mgumu''.

Katika barua yake kwa wizara ya mambo ya nje Kim alisema: '' tangu kuvuja kwa nyaraka za kiofisi kutoka ubalozi huu kumekuwa na hisia kuhusu nafasi yangu na muda wangu uliobaki kama balozi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad