Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa mjumbe wa Umoja wa Afrika, Mohammed el-Hassan Labat, aliyenukuliwa asubuhi ya leo akisema miongoni mwa yaliyokubaliwa ni ratiba ya kipindi cha mpito kuelekea utawala wa kiraia.
Labat amesema pande zote zimekubaliana kuunda baraza huru la pamoja ambalo litaongoza nchi kwa miaka mitatu au zaidi. Pia wamekubaliana nyadhifa tano kwa upande wa jeshi na upande wa raia huku nafasi za nyongeza zikielekezwa kwa raia walio na uzoefu wa kijeshi.
Makubaliano hayo yanaweza kumaliza mkwamo wa wiki kadhaa tangu jeshi lilipomuondoa rais Omar al-Bashir hapo mwezi Aprili.
Mazungumzo ya kugawana madaraka yalivunjika mnamo jeshi lilipowashambulia na kuwaua waandamanaji waliopiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi mjini Khartoum.