Basata Yamruka Amber Rutty " Sio wa Kwetu Hatujawahi Kumsajili Sheria za Mitandao Zichukue Hatua"




Ebwana eh, wakati watanzania walikua washaanza kulisahau sakata la video ya ngono ikimhusisha Amba Rutty na mumewe miezi kadhaa iliyopita.

Wiki hii dude lingine tena likakatisha tena mtandaoni kwa mara ingine na likavuma kama moto wa nyika na sasa bana baraza linalosimamia kazi za sanaa nchini, kutokana na tabia hii limemkana rasmi na kwa waraka mzito.

BASATA imesema haimtambui Amber Rutty kama msanii na hajasajiliwa kufanya shughuli za sanaa kama msanii binafsi au msanii katika kikundi, Baraza limelaani kitendo cha picha zake za faragha kuonekana hadharani na linaamini mamlaka zinazosimamia sheria za mitandao zitachukua hatua.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad