Bibi wa miaka 83 akutwa na hatia ya bangi

Bibi (830 aliyekutwa na gramu 600 za bangi amekutwa na hatia nchini Kenya.

Taarifa zinaeleza kuwa mwanamke huyo alitiwa hatiani jana mbele ya Hakimu Mkazi Nelly Kariuki imeripotiwa na Kituo cha Redio cha Capital FM cha nchini Kenya.

Akiwa mbele ya hakimu Kariuki jana, Lydia Mumbi Ndirangu alikiri kuwa alikutwa na bangi ya thamani ya shilingi za Kenya 500 sawa na shilingi za Kitanzania 12,000  katika eneo la Muthinga, jimbo la Tetu.

Mtuhumiwa ataendelea kushikiliwa na  atatakiwa kurudi tena mahakamani Julai 15 mwaka huu wakati atakaposomewa hukumu.

Kesi inayomkabili bibi hiyo ni ya pili ikihusiana na bangi katika kipindi cha miezi miwili tu nchini Kenya.

Mwezi Mei mwaka huu, Mahakama ya Nyeri ilimhukumu mwanamke mmoja wa makamo, kifungo cha miaka 30 bila faini kwa makosa ya kusafirisha bangi ya thamani ya shilingi za Kenya 2,820  ambazo ni sawa na shilingi za Tanzania 63,000.

Gazeti la daily Nation la nchini Kenya limeandika kuwa inaaminika bibi huyo amekuwa akinunua bangi  mjini Nyeri na kuipeleka kwa mtoto wake wa kiume ambaye huwauzia wateja

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad