Bondia Manny Pacquiao Kuinunua Timu ya Mpira wa Kikapu NBA

BONDIA Mfilipino, Manny Pacquiao, amesema anataka kupigana hadi afikishe umri wa miaka 45 kisha atastaafu na baadaye kununua moja ya timu za ligi ya mpira kikapu nchini Marekani (NBA).
Bondia huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 40 ametengeneza fedha ya kutosha katika masumbwi, hivyo anategemea kuendelea kupigana mnamo miaka mitano ijayo kisha kuning’iniza glovu zake.
“Najihisi kama nina umri wa miaka ya 20 tu,” anasema bondia huyo kwa jina lake maarufu la PacMan au Manny kuonyesha anavyoupenda mchezo huo na mazoezi yanayoambatana nao.

Pacquiao — ambaye atazichapa na nyota asiyewahi kupoteza mchezo wowote,  Keith Thurman, leo (Jumamosi), anasema anahisi amebarikiwa na Mungu na anategemea kukitumia kipaji hicho kiasi mwili wake utakavyomruhusu.
Katika kuonyesha anaupenda sana pia mchezo wa mpira wa kikapu, ameinunua ligi ya mchezo huo huko kwao Ufilipino ambayo inajulikana kama Maharlika Pilipinas Basketball League (MPBL).

Jarida la Forbes linasema Manny ana mkwanja unaozidi Dola mil. 500 (Sh. tril. 1.5) kutokana na masumbwi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad