CCM itahitaji Wajumbe Wapya, Mbinu Mpya 2020


Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi (CCM), kitalazimika kutafuta mbinu mpya za kupata ushindi katika Uchaguzi Mkuu mwakani baada ya timu ya wajumbe 32 iliyofanikisha suala hilo mwaka 2015 kusambaratika.

Timu hiyo iliyokuwa chini ya Katibu mkuu wa wakati huo, Abdulrahman Kinana ilimwezesha Dk John Magufuli kuibuka mshindi wa urais katika uchaguzi huo kwa kupata kura 8,882,935 sawa na asilimia 58.46 huku Edward Lowassa wa Chadema na Ukawa akipata kura 6,072,848 sawa na asilimia 39.97.

Kinana aliyestaafu Mei 2018, anafahamika kutokana na kazi aliyoifanya ya kuongoza kampeni za urais kwa mafanikio, akifanikisha ushindi wa marais wa CCM tangu mwaka 1995, wakati alipoongoza kampeni za Rais Benjamin Mkapa na 2005 wakati Rais Jakaya Kikwete akiingia Ikulu.

Uchambuzi wa Mwananchi  umebaini, idadi kubwa ya wajumbe wa timu hiyo ya kampeni wameshang’atuka, kupangiwa majukumu mengine, kustaafu, kuhama chama na wengine ‘kutumbuliwa ndani ya chama na serikalini na kufariki dunia.

Kutokana na hali hiyo CCM inalazimika kuwa na timu mpya ambayo italazimika kubuni mbinu mpya za ushindi zinazoendana na kile kinachoelezwa na makada kama “CCM mpya”.

By Kelvin Matandiko, Mwananchi kmatandiko@mwananchi.co.tz

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad