Davido Awaburuza Tena Wasanii wa Afrika katika Mapato


Jarida la Instagram Rich List 2019, limetoa orodha ya watu 100 ambao wanaingiza pesa nyingi kupitia matangazo ya biashara wanayopost kwenye kurasa zao za mtandao wa kijamii wa Instagram.


Kutokea barani Africa, Davido ndiye amekuwa msanii wa kwanza anayeingiza pesa nyingi kupitia matangazo anayopost Instagramm ambapo amekamata nafasi ya 38.

Davido analipwa Dola 74,000 sawa na Milioni 170 za Tanzania kwa kila tangazo moja. Pia katika orodha hiyo wapo wasanii kama Wizkid kwenye nafasi ya 46, na Tiwa Savage kwenye nafasi ya 48.

Davido ndiye msanii mwenye wafuasi wengi zaidi katika mitandao ya kijamii ya Instagram na Twitter kutokea barani Africa.  Kwasasa Instagram  ana wafuasi Milioni 11 huku Twitter akiwa na Milioni 5.

Kwa ujumla orodha hiyo inaongozwa na Kylie Jenner, Ariana Grande na Cristiano Ronaldo katika nafasi ya tatu.  Watu wengine maarufu waliopo katika list hiyo ni Kim Kardashian, Beyonce, Lionel Messi, Neymar Jr, Justin Bieber, Nick Minaj, David Beckham na Ronaldinho.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad