Dawa MPYA ya Viagra Kwa Wanawake Kiboko...Wanaume Wapewa Onyo..Msije Bakwa
0
July 03, 2019
Dawa mpya ya viagra kwa wanawake watoa angalizo wanaume wasije kubakwa ndani ya nyumba
Posted On: July 3, 2019 2:06 Pm GMT+0000 Posted By: Beatrice Shayo Comments: 0
Dawa mpya za ukosefu wa hisia za kingono kwa wanawake ijulikanayo kama Viagra ambazo zitaanza kuingia sokoni ifikapo Septemba mwaka huu zimezua gumzo katika mitandao ya kijamii huku wengine wakitoa angalizo wanaume wasije kubakwa.
Baadhi wakichangia mjadala huo walikuwa na hofu isije zikawa na nguvu kubwa kuwashinda wanaume ama kuwataka kufanya mapenzi kinguvu na wengine wakisifia kuwa mambo yatakuwa bomba katika tendo la ndoa.
Juzi Shirika linalohusika na udhibiti wa chakula na dawa nchini Marekani (FDA), liliidhinisha dawa mpya kutibu tatizo la ukosefu wa hisia za kingono miongoni mwa wanawake ambao hawajafikia ukomo wa hedhi.
Ukosefu wa hisia hizo husababishwa na mwanamke kutoshiriki katika vitendo vinavyoweza kuvutia hisia za ngono bila ya kuhisishwa na tatizo lolote.
Kemikali kwa jina Vyleese imejaribiwa kutengeneza kile ambacho kinaweza kuitwa Viagra ya kike.
Hili ni swala tata , kwa kuwa baadhi ya wataalam wanahoji asili ya tatizo la hisia za kingono na kukosoa ukosefu wa msisimko wa mapema wakati mwathirika anapotumia.
Viagra hiyo imetengenezwa na kampuni ya Teknolojia ya Palatin Technologies na kuruhusiwa kuuzwa na Amag Pharmaceuticals.
Viagra hiyo mpya hutumika kupitia sindano ambayo husisimua njia ya akili inayotumika katika hisia za ngono itaanza kupatikana katika baadhi ya maduka ya dawa kuanzia Septemba.
Ikilinganishwa na dawa nyingine, dawa hiyo haifanyi kazi katika mfumo wa mishipa, lakini huongeza hamu ya tendo la ngono katika mfumo wa neva.
Vyleesi itashindana na Addyi ya watengenezaji dawa wa Sprout, dawa ya kila siku ambapo iliidhinishwa 2015 na kwamba watumiaji hawafai kutumia pombe wakati wanapoitumia
Tags