DC atuhumiwa Kuomba Rushwa ya Mil 5


Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, amejibu madai ya kuomba rushwa ya Mil. 5 yaliyotolewa na mmoja wa wafanyabiashara wa Hoteli za Kitalii mkoani Kilimanjaro, katika mkutano wa wadau wa Utalii mkoani humo, ambapo Sabaya mwenyewe amedai suala hilo limeanzia kwenye mgogoro wa ardhi.


Ole Sabaya ametoa kauli hiyo mkoani Kilimanjaro, wilayani Hai, wakati akizungumza na wananchi,  ambapo amesema amekuwa akipokea simu mbalimbali zikimtaka ajibu tuhuma hizo, juu ya matumizi mabaya ya ofisi yake.

Sabaya amesema kuwa "chanzo cha yote hayo ni Bibi aliyelalamika kwangu kuhusu shamba lake kuvamiwa, niliunda Kamati Maalum ambayo iliyoongozwa na Katibu Tawala, Afisa ardhi na Mwanasheria,  waliponiletea taarifa ilionesha Bibi huyo analimiliki tangu 1971."

"OCD nakuelekeza kwa sababu yeye ametoa tuhuma zake akijua leo nakuja kufanya maamuzi, kwanza OCD muhakikishie huyo mfanyanyabiashara Cathibert Swai usalama wake na umtake ajibu mashtaka ya kudhulumu haki za hawa watu" ameongeza Sabaya.

Hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii, kulisambaa kipande cha video kikimuonesha moja ya wafanyabiashara wa Hoteli za Kitalii mkoani Kilimanjaro, aliyefahamika kwa jina la Cathebert Swai akimlalamikia Ole Sabaya kwa matumizi mabaya ya ofisi yake.

Mfanyabiashara huyo alisema kuwa "achana na hiyo mwaka jana mwezi wa 11, alinipa masaa 48 kuhamisha akaunti zangu za benki kwenda Hai bila sababu yeyote, wakati huohuo akawa ananidai fedha ambayo sitakiwi kulipa kwa mujibu wa sheria, na kuna siku alikuja ofisini kwangu akinitaka nimpe milioni 5, nikawa sina budi ikanibidi nimpe tu tena kwa mafungu mafungu."

VIDEO:

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad