Ajali hiyo Jumatatu katika eneo la katikati ya Igunga (Tabora) na Shelui (Singida) ambapo wafanyakazi hao pamoja na madereva wawili waliofariki dunia baada ya basi aina ya Coaster waliokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na gari la mizigo wakati wakielekea wilayani Chato kwa ajili ya uzinduzi wa hifadhi hiyo ya Taifa ya Chato-Burigi.
Katika salamu hizo za rambirambi Rais Shein alieleza kuwa amepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa ya ajali hio na kwamba yeye binafsi pamoja na wananchi wote wa Zanzibar na Tanzania nzima kwa jumla wamejawa na simanzi nzito kutokana na vifo vya wafanyakazi hao.
"Kutokana na msiba huu, natoa salamu za rambirambi kwako Said Salim Bakhressa, ndugu, wanafamilia wa marehemu, marafiki, wafanyakazi wote wa Makampuni ya S.S. Bakhressa pamoja na watazamaji, wasikilizaji na wafuatiliaji wa vipindi na habari mbali mbali zinazotolewa na Azam Media Limited, ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"ilieleza sehemu ya salamu za rambirambi alizozituma Dk Shein."