Dk. Shein kuwa mgeni rasmi Tamasha la Mzanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa tamasha la 24 la Utamaduni wa Mzanzibari litakalofanyika Viwanja vya kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge, mjini Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana,Utamaduni Sanaa na Michezo Amour Hamil Bakari amesema kuwa tamasha hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 19-25 Julai, katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba.

Amesema kuwa tamasha hilo ni la kitaifa, lililoasisiwa mwaka 1995 na aliekuwa Rais wa awamu ya 4 wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Salmin Amour Juma kwa lengo la kulinda, kukuza na kuendeleza utamaduni na Sanaa za Mzanzibari.

Naibu Amour amesema kuwa tamasha hilo litakuwa na sehemu muhimu ya kuonesha kazi na shughuli mbalimbali za utamaduni ili kujenga uwezo na ubunifu katika kukuza vipaji vya Sanaa.

Amefahamisha kuwa tamasha la Mzanzibari lina umuhimu wa kutambua matumizi mazuri ya utamaduni na Sanaa ikiwa ni nyenzo na kuzitangaza bidhaa zenye mvuto na ushawishi katika kusaidia ukuaji wa utalii nchini.

Sambamba na hayo Naibu Katibu huyo alisema kuwa tamasha litatoa fursa kwa Wasanii kuonesha ubunifu na umahiri wa Sanaa zao ili wananchi wapate elimu kupitia Sanaa hizo.

Alisema lengo kuu la Tamasha hilo ni kuwaweka pamoja wasanii wa fani mbalimbali za Sanaa ili kukuza utamaduni wa Mzanzibari kupitia kuonesha Sanaa zao, kubadilishana mawazo na kufurahia utajiri wa urithi wa utamaduni wa jamii ya Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad