Rais wa Marekani Donald Trump ameshutumiwa kwa ubaguzi wa rangu baada ya kundika ujumbe kwenye twitter akiwashambulia wabunge wanawake wa chama cha Democratic.
Amedai kuwa wanawake hao "wamewasili kutoka mataifa ambayo serikali zake ni majanga matupu", kabla ya kupendekeza "warudi walikotoka".
Baada ya hapo alisema kuwa spika Nancy Pelosi "atafurahi sana kuwashughulikia kwa haraka mipango ya safari ya bure".
Haya ni wiki moja baada ya Bi Pelosi kukabiliana kwa maneno na "kundi hilo", la wabunge wasio watu weupe wa mrengo wa kushoto wa chama cha Democratic.
Kati ya wabunge hao wanne, watatu - Alexandria Ocasio-Cortez, Rashida Tlaib na Ayanna Pressley - walizaliwa na kulelewa Marekani, huku wanne, Ilhan Omar, alihamia Marekani alipokuwa mtoto.
Bi Ocasio-Cortez alizaliwa mjini Bronx - New York, kiasi cha maili 12 kutoka hospitali ya Queens alikozaliwa Trump mwenyewe.
Rais Trump amesema nini?
Katika msururu wa ujumbe kwenye twitter, Trump amewashutumu wabunge hao kwa kumshutumu yeye na Marekani kwa "ukali".
Aliandika: "Inavutia kuona wabunge wa Democratic 'wanaotaka maendeleo' ambao waliwasili kutoka nchi ambazo serikali zake ni majanga matupu, zilizo mbaya zaidi, zilizo na kiwango kikubwa cha rushwa, na zisizojiweza kokote duniani (iwapo ni serikali zilizokuwa zinafanya kazi) sasa wakizungumza kwa ukali wakiwaambia watu wa Marekani, taifa kubwa na lenye nguvu duniani, namna tunavyostahili kuiendesha serikali yetu.
"Kwanini wasirudi kusaidia kuyarekebisha mataifa yaliosambaratika na yaliogubikwa kwa uhalifu wanakotoka. Alafu warudi watuonyeshe namna inavyostahili kushughulikiwa.
"Maeneo hayo yanhitaji usaidizi wenu sana, mungeondoka haraka sana. Nina hakika Nancy Pelosi atafurahi sana kuwashughulikia mipango ya safari ya bure!"