Emirates Kurejesha Safari Zake Sudan

Emirates Kurejesha Safari Zake Sudan
Shirika kubwa kabisa la ndege katika Mashariki ya Kati, Emirates Airline, limesema leo kuwa limeamua kuanzisha tena safari kwenda Sudan kuanzia Julai 8 baada ya kusitisha kwa mwezi mmoja kutokana na machafuko yaliyosababisha umwagikaji damu.

Taarifa ya Emirates imesema kuwa wamechukua uamuzi huo baada ya kufuatilia kwa karibu hali nchini Sudan na kutathmini kwa kina mazingira yote ya uendeshaji huduma.

Emirates itakuwa na safari moja ya ndege kila siku nchini Sudan. Viongozi wa maandamano wameingia katika siku ya pili ya mazungumzo na watawala wa kijeshi yakiwa ni ya kwanza ya aina yake kuwahi kufanyika tangu kushambuliwa kwa waandamanaji mwezi uliopita.

Kiongozi mmoja wa waandamanaji, Ahmed al-Rabie amesema kuwa mazungumzo ya leo yanajikita katika suala la nani ataongoza baraza huru la mpito. Mpango wa Ethiopia na Umoja wa Afrika unatoa wito wa kuundwa baraza litakaloongozwa na raia wengi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad