Familia ya Msaidizi wa Membe Yaomba Msaada

Familia ya Msaidizi wa Membe Yaomba Msaada
Familia ya  msaidizi wa Bernard Membe, Allan Kiluvya anayedaiwa kutekwa usiku wa kuamkia Julai 7, imeomba msaada baada ya kufanya jitihada za kumtafuta vituo mbalimbali vya polisi jijini Dar Es Salaam bila mafanikio.

Ndugu hao wamejitokeza leo Julai 8, kuomba msaada kwa Rais Dkt John Magufuli, Serikali na watanzania kwa ajili ya kufanikisha kumpata.

Akizungumza kwa niaba ya Familia, Mjomba wa Allan, Samwel Ng'andu amesema kutokana na jitihada walizozifanya lakini sasa wameshaanza kukata tamaa ya wapi watampata ndugu yao, na kueleza ni mazingira yapi aliyotekwa Allan.

''Alikuwa kwenye matembezi ya jioni na dada zake, wakati anawarudisha nyumbani, alipowafikisha na kutaka kutoka, ile anageuza gari, ghafla ilitokea gari ikamblock kwa nyuma kiasi ambacho alishindwa kugeuza, na kwa sababu alikuwa amekunywa kidogo oviousily alikasirika, kidogo alishuka na kisha dereva walile gari jingine alishuka''

Mjomba wa Allan aliendelea kueleza, ''Ghafla akawa amezungukwa na watu sita, na ndipo walipomvamia Allan, na akaanza kuomba msaada kwa dada yake Magreth, Magreth naomba unisaidia, Magreth naomba unisaidie!! na Magreth alipoonyesha dalili ya kupiga kelele, mmoja alitoa bastola na kumuwekea kichwani''

Baada ya Magreth kuanza kupiga kelele, na ndipo ndugu wengine walipoamka na kukusanyana kwenda, kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi cha kawe majira ya saa 8 usiku.

Aidha wametoa wito kwa viongozi mbalimbali wa dini, kuendelea kumuombea Allan ili kokote aliko akaweze kuwa salama.

Kwa mujibu wa wanafamilia, gari iliyomteka Allan ni Land Cruiser yenye namba za usajili T 810 BQS rangi ya kijivu na gurudumu lake limefunikwa na rangi ya chungwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad