Fatuma Karume Aliamsha Dude



Wakili Fatma Karume amesema Rais John  Magufuli ametuma ujumbe mkubwa kwa mababa kuwa watoto wao hawatabaki kuwa mawaziri, wabunge ama makatibu wakuu.

Fatma aliyasema hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter kuwa leo Rais Magufuli ametuma message kubwa kwa mababa.

Aliandika ujumbe unaosomeka hivi :
“Leo Magu katuma message kubwa kwa mababa. Thubutu na mtaona  kama watoti wenu watabaki kuwa mawaziri, wabunge, makatibu wakuu Message sent and delivered kwa wazee,”


Leo, Rais John Magufuli amefanya uteuzi wa mawaziri wapya wawili, akimteua Hussein Bashe kuwa naibu Waziri wa Kilimo kuchukua nafasi ya Innocent Bashungwa ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

Pia, amemteua George Simbachawene kuchukua nafasi ya aliyekuwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba, ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad