Filamu za Kutafsiri Sasa Basi..Faini Kubwa Kutolewa


Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Doreen Sinare amesema watu ambao wanadurufu na kuuza  kazi ambazo sio zao ziwe za Tanzania au nnje ya nchi na za kutafsiri zote ni kazi za kiharamia.

Hayo ameyasema janaa Julai 1 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa Habari na kuongeza kua endapo wakizikuta kazi hizo hasa zinazotafsiriwakwa uongo, watazibeba na muhusika kulipa usumbusu na gharama za kufuatwa.

Amesema Sheria mpya ikianza kufanya kazi basi matekelezo yataanza  ambapo kwa sasa wanasubiri Mh. Rais aweze kuridhia adhabu zilizopendekezwa.

Amesema, adhabu iliyokuwepo awali kwenye Sheria ilikuwa ndogo ambapo mtu akikutwa na kosa la jinai kwenye haki miliki alikua anaweza kutozwa pesa isiyozidi Milioni 5 au kifungo cha miaka mitatu na  kama amerudia mara ya pili ni milioni 10 au miaka 5.

“Kwa sasa tumeiongeza na kufika Milioni 20 kwa kosa la kwanza, na kosa la pili milioni 30, lakini wote hao ikitokea tumeenda kwenye eneo la tukio na mali tuliyoikuta ni zaidi ya kile kiwango cha kwenye sheria basi tunaweza kufanya mara tatu ya ule mzigo ambao tumeukuta pale,” amesema

Ameongeza kuwa, Sheria imetoa Mamlaka kwa Cosota kuweza kuwatoza papo hapo wale ambao watakutwa wamekiuka Sheria na kukiri kwamba ni kweli wamekosea.

Amesema, mambo hayo yameingizwa kwenye marekebisho ya Sheria wiki iliyopita tu na  sasa wanasubiri utekelezaji wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad